Writen by
sadataley
1:25 PM
-
0
Comments
Na Mussa Juma, Mwananchi
Arusha. Serikali imesisitiza uamuzi wake wa kupiga marufuku uingizwaji nchini wa kuku, nyama ya kuku na vifaranga ili kudhibiti ugonjwa ya mafua ya ndege na kulinda wawekezaji wa ndani.
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus
Kamani alitoa agizo hilo baada ya kutembelea kampuni ya Tanzania Poulty
Farms Limited, inayomiliki shamba la kuku wa nyama na vifaranga lililopo
kijiji cha Ngogongare na kiwanda cha uchinjaji kuku kilichopo Mbuguni
wilayani Arumeru.
Waziri Kamani alisema Serikali ilipiga marufuku
uingizwaji wa kuku wa nyama na vifaranga kutoka nje kutokana na magonjwa
ya mafua ya kuku na haijaruhusu uingizwaji huo kwa lengo la kunusuru
soko la wazalishaji wa ndani .
“Serikali haijawahi kutoa vibali vya uingizaji wa
kuku wala nyama kutoka nje, ili kunusuru wazalishaji wa ndani, na
kulinda ajira za wananchi,” alisema
Aaliwapongeza wamiliki wa shamba hilo kwa kutumia
teknolojia ya kisasa katika kuwahudumia kuku, utengenezaji wa chakula
cha kuku, kufuga hadi kuchinja na kuhifadhi kwenye majokofu kwa ajili ya
kusafirisha kwenda sokoni.
‘’Hii ni teknolojia ya kwanza na ya kisasa
kutumika hapa nchini ya kuwahudumia kuku, kuzalisha chakula, kufuga na
kuwachinja na kisha kusambaza kwenye soko,’’ alisema
Awali mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tanzania
Poultry Farms Limited, Amin Bathawab alisema walianza uwekezaji mwaka
1996 baada ya kuinunua iliyokuwa kampuni ya taifa ya kuku, Napco, ikiwa
na kuku 2,000.
Alisema hadi sasa wana kuku wazazi 80,000 na vifaranga 90,000. Hivi sasa wanauza vifaranga nchi nzima kupitia kwa mawakala.
No comments
Post a Comment