Writen by
sadataley
1:36 PM
-
0
Comments
Na Mwandishi wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetenga Sh6 bilioni kukopesha vijana kufanya shughuli za ujasiriamali.
Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Femina Hip
ulioshirikisha vijana kutona shule mbalimbali nchini, Kaimu Mkurugenzi
wa Vijana, James Kajugusi alisema fedha hizo zitakopeshwa kwa vijana
kupitia vyama vya ushirika vilivyopo halmashauri.
“Tutatoa fedha hizi kupitia Saccos, vikundi vya
vijana viainishe mpango kazi wa kujiajiri ambao utatufikia na
kuupambanua, tukiona una manufaa kwa taifa basi tutaoa mkopo wenye riba
nafuu,” alisema Kajugusi.
Alisema tayari Serikali imepokea zaidi ya maombi 3,000 ambayo wanayapitia ili kutoa mikopo.
Alisema vijana inabidi wajiajiri wenyewe bila
kutegemea kuajiriwa kwa kutumia elimu waliyonayo, fursa za maendeleo
zinazowazunguka maeneo yao.
“Tanzania tuna idadi ya vijana milioni 16.2 na
kila mwaka vijana milioni 2 wanaomba ajira sekta ya umma, lakini ni
takriban 100,000 wanaoajiriwa na wengine wanajiajiri wenyeye,” alisema.
Katika mkutano huo, Femina Hip ilizindua logo yake
mpya na kutoa zawadi kwa Mwalimu Gaudence Mhando wa Sekondari ya
Wasichana ya Iringa, kwa kuchochea maendeleo kwa wanafunzi wake kupitia
klabu yao ya Fema iliyopo shuleni hapo.
No comments
Post a Comment