Writen by
sadataley
10:28 PM
-
0
Comments
Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Rwanda
amethibitisha kuwa serikali inawafukuza maafisa sita wa ubalozi wa
Afrika Kusini, saa chache baada ya Afrika Kusini kuwataka raia watatu wa
Rwanda kuondoka nchini humo.
Afrika Kusini ilichukua hatua hiyo baada ya
nyumba ya mpinzani mmoja wa Rwanda anayeishi Afrika Kusini kushambiliwa
siku ya Jumaane.Jenerali Kayumba Nyamwasa, ambaye aliwahi kuwa mkuu wa majeshi nchini Rwanda, hakuwa nyumbani wakati wa shambulio hilo.
Nyumba yake iliharibiwa na komputa na baadhi ya nyaraka zilichukuliwa.
Jenerali Nyamwasa amenusurika na majaribio mawili mengine ya kumuuwa akiwa Afrika Kusini.
Tayari watu wanafanyiwa kesi ya kujaribu kumuuwa - wakiwemo Wanyarwanda watatu na Watanzania watatu.
Source:bbc
Imewelwa na Kelvin Peter
No comments
Post a Comment