Writen by
sadataley
9:47 PM
-
0
Comments
Zifuatazo ni picha za ajali iliyohusisha magari matatu siku ya Alhamisi,
(6 Machi 2014) eneo la Bwawani, barabara kuu iendayo Morogoro, ambapo
gari la mafuta aina ya Iveco lenye namba za usajili T272 ASB, mali ya
kampuni ya OilCom imeripotiwa kugongana uso kwa uso na gari la abiria,
Tata, Linowele Classic lenye namba za usajili T252CHN lililokuwa
likitokea Dar es Salaam kwenda Malinyi pamoja na gari nyingine ya abiria
la Adventure, lenye namba za usajili T335CCD, Nissan Diesel
iliyoripotiwa kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kigoma.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wanaeleza kuwa ni mwendo wa gari
la Linowele, ambapo dereva wake alishindwa kuumudu kutokana na mvua
zilizokuwa zinanyesha, na hivyo kupelekea kulivaa lori la mafuta, ambapo
dereva wa lori amefariki dunia. Kwa upande wake, dereva wa basi la
Linowele ameripotiwa kubanwa na usukani na kupelekea kuvunjika mguu,
ambapo askari magereza walifanikiwa kutoa msaada mkubwa kwa majeruhi
wanaoripotiwa kufikia 38.
Kwa maelezo ya mashuhuda, basi la adventure nalo wakati likija kwa
mwendo kasi kukaribia eneo la tukio, jitihada zilifanywa na askari
kulisimamisha ili lisipate kuyavaa magari hayo mawili, ambapo kuona
hivyo, dereva wake alilazimika kukwepesha na kisha kuliingiza mtaroni.
Zifuatazo ni picha za tukio lote.
Wananchi wakitazama mabaki ya gari la abiria, Linowene iliyokuwa ikielekea Malinyi, Morogoro kutokea Dar es Salaam
Dereva wa lori, Scania, mali ya kampuni ya Twiga Cement akijiandaa
kuvuta gari la Linowene, kabla ya kuachia kijiti kwa lori lingine
kuiyuta kwa pembeni, nje ya barabara.
Taswira kwa mbali ikionyesha basi la Linowele na Adveture, ambapo lori aina ya Scania likiivuta kuiondoa barabarani
Mwili wa dereva wa gari la mafuta, mali ya kampuni ya OilCom.
Sehemu ya foleni kwenye eneo la tukio.
HABARI NA PICHA NI KWA HISANI YA GOSPEL KITAA
Imewekwa na Kelvin Peter
No comments
Post a Comment