Writen by
sadataley
11:56 AM
-
0
Comments
Na Mwananchi
Dar es Salaam. Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imetangaza kusitisha mgomo wa wafanyabiashara uliodumu kwa takriban siku tano kupinga notisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuwapa siku 14 za kufunga Mashine za Elektroniki za Kutoza Kodi (EFD).
Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Patrick Masagati alisema jana kuwa mgomo huo umefutwa baada ya makubaliano baina yao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku akisema kimsingi hawapingi matumizi ya mashine za EFD, isipokuwa mfumo mzima wa utozaji kodi nchini.
jana kuwa mgomo huo umefutwa baada ya makubaliano baina yao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku akisema kimsingi hawapingi matumizi ya mashine za EFD, isipokuwa mfumo mzima wa utozaji kodi nchini.
“Waziri Mkuu, Pinda amesitisha notisi ya TRA ya siku 14 na ameahidi kuunda chombo kitakachopitia mfumo mzima wa kodi nchini,” alidai Masagati.
Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mazungumzo hayo na Mwandishi wake wa Habari, Irene Bwire hakupatikana pia kuzungumzia suala hilo.
Makamu huyo wa JWT alidai kuwa Waziri Mkuu aliahidi kuchukua hatua stahiki kwa haraka baada ya kukutana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya na watendaji wa TRA.
Masagati alisema katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wenyeviti wa jumuiya hiyo kutoka mikoani, pia walimfahamisha Waziri Mkuu kuhusu mianya ya rushwa ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Aidha, alisema walimfahamisha jinsi matumizi ya EFD yanavyosababisha vishawishi vya rushwa miongoni mwa watendaji wa TRA na kero nyingine wanazokumbana nazo, hali ambayo inakwaza biashara zao na kuwakwamishia juhudi zao za kujiongezea kipato.
Mgomo wa wafanyabiashara wenye maduka ulianza Jumapili iliyopita kushinikiza kuondolewa kwa notisi ya siku 14 iliyotolewa na TRA ikiwataka kununua na kutumia mashine hizo katika biashara zao.
Kutokana na tangazo hilo, wafanyabiashara sehemu mbalimbali nchini walitangaza mgomo wa kufanya biashara hadi pale Serikali itakapositisha amri hiyo.
Akizungumzia taarifa hizo za kusitisha mgomo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema jana kwamba ofisi yake haina taarifa juu ya mkutano huo wa wafanyabiashara na Waziri Mkuu.
Hata hivyo, alisema endapo wamekubaliana kusitisha mgomo ni jambo jema na la kizalendo.
No comments
Post a Comment