Writen by
sadataley
10:05 PM
-
0
Comments
WAFILIPINO WAMUOMBA MUNGU KUWAONDOLEA MAJANGA
![]() |
Kanisa la Mtakatifu Ignatius wa Loyola Parish katika mji wa Medellin Cebu likiwa bila paa baada ya kimbunga hicho.©Gma News. |
Kimbunga kinachoitwa Typhoon Yolanda kimeleta madhara makubwa katikati na kusini mwa nchi ya Ufilipino watu zaidi ya 1000 wamepoteza maisha pia kimeharibu mali mbalimbali za watu. Kutokana na kimbunga hicho watu mbalimbali wa nchi hiyo wamekuwa wakimiminika makanisani kumuomba Mungu awaondolee majanga pamoja na kuwatia moyo watu waliokumbwa na tatizo hilo.
Aidha askofu mkuu wa jimbo la Cebu kanisa katoliki Jose Palma amewataka wafilipino kumuomba sana Mungu ili kuwaondolea majanga, ikiwa pia kuwashirikisha wenzao kwenye mitandao ya kijamii kuiombea nchi hiyo. Ufilipino taifa la Kikristo asilimia kubwa wakiwa wakatoliki, limekuwa likikumbwa na majanga kila mwaka yakiwemo matetemeko ya ardhi, vimbunga pamoja na mafuriko.
Baadhi ya wananchi wa Ufilipino wakiwa kanisani kumuomba Mungu. |
![]() |
Baadhi ya wanachi wa Ufilipino wakiwa katika mstari wa kwenda kuchukua msaada wa chakula.©gmanews |
No comments
Post a Comment