Writen by
sadataley
9:23 PM
-
0
Comments
Na Godfrey Kahango, MwananchiMbeya.Tanzania na Malawi zimeandaa mpango wa pamoja kujenga mabwawa matatu makubwa kandokando mwa Mto Songwe ulio mpakani mwa nchi hizo, ili kutunza maji yanayosababisha mafuriko kipIndi ch mvua na kuwaathiri wakazi wa nchi hizo wanaoishi karibu na Ziwa Nyasa.
Taarifa hiyo ilitolewa na waratibu wa kuendeleza
Mradi wa Bonde la Mto Songwe kutoka nchi hizo juzi kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini
kilichofanyika jijini hapa.
Mratibu wa mradi huo kwa upande wa Tanzania,
Gabriel Kalinga ambaye aliambatana na mratibu mwenzake kutoka Malawi,
Erick Chidzungu, alisema mradi huo ulibuniwa ili kuondokana na adha ya
mafuriko inayowakumba wakazi wa nchi hizo eneo la bonde la mto huo
karibu na Ziwa Nyasa.
Alisema mbali na hatua hiyo pia ni njia mojawapo
ya kuwekeza vitegauchumi kwa nchi zote kwani mabwawa hayo yanaweza
kutumika kuzalisha umeme na pia kufanya kazi za umwagiliaji katika ekari
zinazokadiriwa kufikia 3,000.
Wilaya zinazopitiwa na mto huo ni Mbeya Vijijini,
Ileje , Kyela na kwamba kwa upande wa Malawi zipo wilaya zilizo karibu
na mto huo.
Kalinga alisema hadi hatua hii tayari Benki ya
Maendeleo ya Africa (ADB) imekubali kwamba mradi huo una manufaa makubwa
na kuongeza kuwa unaweza kutekelezeka.
No comments
Post a Comment