Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, November 11, 2013

Ni wakati wa Tanzanite kuweka historia mpya

Hivi sasa vijana wa Tanzanite wameingia raundi ya pili, ambapo watakabiliana na Afrika Kusini ambayo imefika raundi hiyo baada ya kuichapa Botswana 7-2. 
Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite’ iliwasili jana ikitokea Maputo ilipokuwa kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji kuwania tiketi ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa wanawake chini ya miaka 20.
Fainali hizo za dunia kwa wanawake chini ya miaka 20 zitafanyika Canada mwakani kuanzia Agosti 5-24, ambapo timu 16 zitakazofuzu kutoka mashirikisho sita duniani zitashiriki fainali hizo.
Tayari vijana wa Tanzanite wameingia raundi ya pili ya kuwania kufuzu fainali hizo za kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 20 kwa upande wa nchi za Afrika kwani waliichapa Msumbiji 10-0 katika mechi iliyochezwa jijini Dar es Salaam na katika mechi ya marudiano huko Maputo walishinda 5-1.
Hivi sasa vijana wa Tanzanite wameingia raundi ya pili, ambapo watakabiliana na Afrika Kusini ambayo imefika raundi hiyo baada ya kuichapa Botswana 7-2.
Mechi hizi za raundi ya pili zitachezwa Desemba 6 na kurudiana Desemba 20, ambapo kama vijana wa Tanzanite watafanya vizuri basi wataingia raundi ya tatu ambayo ni raundi ya mwisho ambayo itachezwa Januari 10 na mechi za marudiano zitachezwa Januari 24, 2014.
Vijana wa Tanzanite wanahitaji maandalizi mazuri ili kuendeleza rekodi yao ya kufanya vizuri katika mashindano haya ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa sababu wanayo kila sababu ya kufanya vizuri kwani wanaonyesha nia hiyo.
Ili kuiwezesha Tanzanite kuwa na maandalizi mazuri, Watanzania tunatakiwa kuisaidia kwa kila hali timu hii ili isifanye maandalizi ya wasiwasi kwa sababu Tanzanite imeonyesha ikisaidiwa ina uwezo wa kuliletea furaha Taifa.
Tunatakiwa tuisaidie hivi sasa kwa sababu itakuwa haina maana kama tukisubiri ifuzu ndiyo tuisaidie, huu ndiyo wakati mwafaka kujitokeza na kuisaidia Tanzanite kwa nguvu zote ili kuiweka timu yetu katika mazingira mazuri ya kufanya vizuri.
Sisi tunaamini vijana wa Tanzanite wana uwezo mkubwa na wanaweza kufanya vizuri zaidi kwani timu ya Tanzanite inaundwa na vijana wengi walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika Nigeria na kutwaa ubingwa wa Afrika.
Tunajua kwamba bado vijana wa Tanzanite wana safari ndefu na ngumu ya kuhakikisha wanafuzu fainali hizo za dunia za vijana chini ya miaka 20, lakini kama Watanzania tutawasaidia vijana hawa wa Tanzanite, kila kitu kitawezekana kwao.
Sisi tunaamini vijana wa Tanzanite wana uwezo mkubwa wa kuishangaza dunia, lakini wanakosa motisha kama vile mechi za kirafiki za kimataifa pamoja na kutunzwa vizuri kwa sababu tu ya hali ya kiuchumi. Hata hivyo tunaamini Shirikisho la Soka Tanzania TFF litahamasisha wadau mbalimbali waweze kujitokeza kuisaidia Tanzanite kwa sababu hali inavyoonekana jamii haijashawishiwa kukubali kwamba Tanzanite wanaweza kufuzu fainali za dunia chini ya miaka 20.
Pia tunaamini Watanzania wengi watajitokeza uwanjani kuiunga mkono Tanzanite itakapokuwa inacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Desemba 6 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tunaamini kwamba vijana wa Tanzanite wana uwezo wa kupigana hadi dakika ya mwisho na kuandika historia mpya katika soka la wanawake Tanzania. Vijana hawa wanaweza.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment