Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, November 8, 2013

Mpelelezi wa ki-Palestina asema Israel ndio mshukiwa mkuu wa kifo cha Arafat.
Kiongozi wa zamani wa  Palestina hayati  Yasser Arafat.
Kiongozi wa zamani wa Palestina hayati Yasser Arafat.
Mpelelezi wa ki-Palestina anasema Israel ndio mshukiwa wa kwanza  mkuu na  pekee wa  kifo cha rais Yasser Arrafat, baada ya wanasayansi wa Uswiss kusema kuwa kulikuwa na ushahidi wa kiasi kuwa alipewa sumu  yenye mnunurisho.

Tawfik Tirawi mpelelezi mkuu wa ki-Palestina  anayechunguza  kifo cha Arafat aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa  huko Ramaallah kwamba uchunguzi utaendelea alikielezea kifo cha Arafat kuwa ni uhalifu wa karne ya 21.

Maelezo hayo yametolewa baada ya wanasayansi wa ushahidi wa Uswiss  kusema kuwa wamepata ushahidi wa kiwango fulani unaounga mkono wazo  kwamba kiongozi huyo wa Palestina  alipewa sumu inayosababisha kifo ya mnunurisho wa Polonium.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment