Writen by
sadataley
9:14 PM
-
0
Comments
Na Elias Msuya, MwananchiDar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Tanzania iko tayari kujitoa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani kuna kila dalili ya kutengwa.
Mpasuko wa jumuiya hiyo umejidhihirisha siku za
karibuni baada ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kufanya mikutano na
kuafikiana kwa mambo kadhaa, huku nchi za Tanzania na Burundi
zikitengwa.
Akijibu maswali ya Wabunge hivi karibuni Bungeni
mjini Dodoma, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
alisema bado Tanzania inatafakari mwenendo huo na inasubiri mkutano wa
Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Jumuiya hiyo wiki mbili zijazo ili
itoe msimamo wake.
Hata hivyo akizungumza na kituo cha Channel Ten
juzi jijini Dar es Salaam, Waziri Membe alisema Tanzania iko tayari
kujitoa na haitapata hasara yoyote.
“Iko wazi tu kwamba tumeshatengwa na
wenzetu...inaweza kuwa sababu pengine tumepeleka majeshi yetu Mashariki
ya Jamhuri ya Kidemokrasiamya Congo kuwachakaza, au pengine inawezeka
kuna mtu anataka awe kiongozi (Rais) wa Afrika Mashariki na wengine
tukakataa mpango huo.”
“Sisi hatutakubali kuburuzwa,” alisema Membe.
No comments
Post a Comment