Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, November 6, 2013

Kongamano la amani Syria laahirishwa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika jumuiya ya nchi za kiarabu, amesema 
kuwa kongamano la amani kuhusu Syria lililokuwa limepangwa kufanyika mjini 
Geneva mwezi huu , limeahirishwa.

Lakhdhar Brahimi anasema atahakikisha mkutano unafanyika angalu kabla ya mwisho wa mwaka

Mjumbe huyo Lakhdar Brahimi hata hivyo amesema kuwa angali ana matumani ya kufanyika kongamano la amani ifikapo mwishoni mwa mwaka.Amesema kuwa baada ya kukutana na wanadiplomasia wakuu, hakuwa tayari kutangaza tarehe ya mkutano huo.
Juhudi za kuandaa kongamano kati ya serikali na wapiganaji nchini Syria, zimekuwa zikiendelea kwa miezi kadhaa sasa baada ya kutokwepo maelewano kuhusu nani ahudhurie mkutano huo pamoja na ajenda ya mkutano wenyewe.
Bwana Brahimi amesema atakutana wanadiplomasia wa Marekani na Urusi kwa mara nyingine tarehe 25 , Novemba.
"Tulitumai kuwa tungeweza kutangaza tarehe ya mkutan huo leo, lakini ka bahati mbaya hilo halitafanyika,’’ Brahimi aliambia waandishi wa habari.
Mjumbe huyo aliongeza kusema kuwa hakuna kikubuwa kilichofanyika katika mazungumzo yaliyofanyika Jumanne na kwa kwamba sio ajabu tarehe ya mkutano haikuamuliwa.
Brahimi alikutana na mawaziri wa Marekani na Urusi na kisha baadaye kukutana na wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Uingereza, Ufaransa, na China pamoja na chi jirani za Syria, Lebanon, Iraq, Jordan na Uturuki.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment