Writen by
sadataley
1:11 PM
-
0
Comments
Siku moja baada ya Serikali ya Kenya kutangaza kuwa itaendelea kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, wachambuzi wa masuala ya siasa bado wanaona kuwa viongozi wa Afrika wanataka kujitoa kwenye mkataba wa Roma kwa maslahi yao binafsi.
Msimamo wa Kenya kushirikiana na mahakama ya ICC unatolewa licha ya maazimio ya viongozi wa Umoja wa Afrika Au kumtaka rais Kenyatta na naibu wake William Ruto kutohudhuria vikao vyao kwa kile umoja huo unadai mahakama ya ICC haitendi haki kwa viongozi hao.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa hatua ya viongozi wa Umoja wa Afrika kutaka kujitoa kwenye mkataba unaotambua mahakama ya ICC ni njia nyingine ya kutaka kuficha makucha yao kwakuwa ni vinara wa kukiuka haki za binadamu.
Mwishoni mwa juma viongozi wa Umoja wa Afrika waliokutana mjini Addis Ababab, Ethiopia kwa kauli moja walikubaliana kuiandikia barua mahakama ya ICC na baraza la Umoja wa mataifa UN kutaka kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ziahirishwe mpake pale watakapomaliza muda wao wa uongozi.
Viongozi hao walikubaliana Kuanzia sasa hakuna Kiongozi wa nchi yoyote ya Afrika atakayepelekwa ICC au Mahakama yoyote wakati akiwa madarakani,Kiongozi yoyote yule ambaye Katiba inamruhusu kukaimu Urais naye hatapelekwa ICC akiwa madarakani, Viongozi wa Afrika wanaotuhumiwa makosa washtakiwe baada ya kumaliza mihula ya uongozi.
Viongozi wa Afrika wamesikitishwa na mwenendo wa ICC, toka 2004, kati ya kesi 30, kesi 27 ni kutoka nchi za Bara la Afrika, Kuhusu Afrika kujitoa ICC, Wakuu wa AU wamekubaliana ni mapema mno na itategemea matokeo ya mkutano wa Rome Statue utakaofanyika Nov, 2013.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa licha ya makataa hayo kunauwezekano mdogo wa Umoja wa Mataifa UN kukubaliana na maombi haya mapya ya AU kutaka kesi hizo kuahirishwa kwasababu mbalimbali ikiwemo swala la usalama nchini Kenya.
Maazimio ya Umoja was Afrika yanakuja ikiwa imepita miezi kadhaa toka mahakama ya kimataifa ya ICC itupilie mbali ombi la umoja wa Afrika kutaka kesi hizo ziahirishwe kwa madai zinawalenga viongozi wa Afrika pekee.
No comments
Post a Comment