Writen by
sadataley
1:13 PM
-
0
Comments
Raisi wa Iran Hassan Rouhani amekuwa akisisitiza kuwa mpango wa nyuklia ya Iran ni mpango wa amani
Raisi wa Iran Hassan Rouhani amekuwa akisisitiza kuwa mpango wa nyuklia ya Iran ni mpango wa amani
Viongozi kutoka Mataifa yenye nguvu duniani hii leo wanatarajiwa kukutana mjini Geneva Uswis kujaribu kuwa na mazungumzo mapya na nchi ya Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia,Mazungumzo haya ya siku mbili yanatarajiwa kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na nchi ya Iran kuhusu mpango wke wa nyuklia na namna inavyopanga kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.
Balozi wa Iran nchini Ufaransa Ali Ahani amesisitiza utayari wa nchi yake kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kama rais Hassan Rowhan alivyoahidi.
Kwa upande wake mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya EU Catherine Ashton anaona kuwa huenda mazungumzo ya safari hii yakazaa matunda licha ya changamoto zilizoko.
Aidha afisa mmoja wa juu wa Marekani amewaambia wanahabari kuwa hakuna matarajio ya kupatikana suluhu wakati ambao Iran imeendelea kusisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani.
Wajumbe wa Marekani katika mazungumzo hayo ni pamoja na mmoja ya mtaalam wa vikwazo kutoka Marekani Adam Szubin, ambaye ni mkurugenzi katika idara moja nyeti nchini Marekani.
No comments
Post a Comment