Writen by
sadataley
8:19 PM
-
0
Comments
Huku matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu yakisubiriwa, tume ya uchaguzi ya Zimbabwe inasema chama cha Rais Robert Mugabe, ZANU-PF, kimepata theluthi mbili za viti.
Inamaanisha ZANU-PF ina viti vya kutosha kuweza kubadilisha katiba.
Mpinzani mkuu wa ZANU-PF, chama cha MDC, kimekuwa na kikao kuamua mikakati ya siku za usoni.MDC inasema haitakubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu ya udanganyifu mkubwa katika upigaji kura.Inaarifiwa kuwa afisa mmoja wa tume ya uchaguzi amejiuzulu, na ametaja ulalamishi katika kura.Makundi mawili ya Afrika ya wasimamizi wa uchaguzi, kwa jumla yameunga mkono uchaguzi ingawa yameeleza wasi-wasi kuhusu idadi ya wapigaji kura bandia, na kwamba baadhi ya wapigaji kura hawakuruhusiwa kupiga kura.
Imewewa na Happy Adam
No comments
Post a Comment