Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, August 21, 2013

UVCCM yamtaka Rais Shein amtimue kazi Mwanasheria Mkuu Z`bar (wengine waonekane na wao wamo kumbe njaa inawasumbua kina shaka hao)

                                            Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)  imemtaka  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Othman Masoud Othman, kufuatia matamshi yake  yanayokinzana na kupingana na dhamana aliyopewa na Rais kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukivunjika haitokuwa kiroja.
Msimamo huo wa UVCCM ulitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya jumuiya hiyo Zanzibar yaliyopo Gymkhana, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Alisema matamshi ya Othman kutaka muundo wa muungano wa serikali tatu yamesigana na dhamana aliyopewa pamoja na kukiuka amana ya kimajukumu ya kikatiba aliyopewa ya kusimamia na kuitetea ipasavyo serikali ya Zanzibar.
Alisema kitendo cha kushiriki kongamano na kujitambulisha kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku akiweka msimamo na kupendekeza muundo wa serikali tatu badala ya mbili, ni kukiuka na kuvunja maadili ya ajira yake.
“Othman kama kweli ni muungwana, anayeheshimu utetezi na msimamo wake wa kushabikia muundo wa serikali tatu badala ya mbili zilizopo aonyeshe ujasiri na kujiondoa serikalini mara moja” alisema wakati akisoma tamko la jumuiya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM huyo alisema ni kunyume na taratibu kwa msaidizi wa Rais upande wa masuala ya sheria aliyeapa kumsaidia, kulinda Katiba ya Zanzibar, kuitetea na kuihifadhi akipita njia tofauti ya kisera na Rais wake.
Shaka alisema ni vyema Othman akaipinga SMZ akiwa nje kwani  akibaki ndani ya chombo hicho kazi yake si kupinga bali ni kushauri au kuzungumza baada ya kushauriana na Rais.
“Aueleze umma ametumwa na nani kutoa msimamo wa muungano wa serikali tatu, SMZ na SMT hazijatoa misimamo yake,  CCM ina sera ya muundo wa serikali mbili na CUF tatu, Mwanasheria Mkuu anapozungumzia tatu ametumwa na chama gani?” alihoji Shaka.
Alisema kutokana na misimamo hiyo ya Othman inayoenda kinyume na sera za chama chake na ipo haja kwa Rais, Dk. Shein kumfukuza kazi kwa kitendo chake cha usaliti na kubeza matakwa ya kisera ya Rais aliyemteua na kumpa dhamana ya nafasi alionayo.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alipoulizwa ikiwa Rais na Mwanasheria Mkuu  watakataa kutimiza wito wao jumuiya itachukua hatua zipi, alisema UVCCM imejipanga kufanya  maandamano makubwa ya amani ya kumshinikiza Rais amuondoe Mwanasheria Mkuu huyo serikalini kutokana na kitendo chake cha kuchafua hali ya hewa ya kisiasa ya Zanzibar.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment