Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, August 21, 2013

JK: KUNA UHABA WA WAHADHIRI

RAIS Jakaya Kikwete, amevitaka vyuo vikuu kutoa fursa za kutosha kwa wanafunzi wanaochukua Shahada za Uzamili na Uzamivu, ili kupunguza tatizo la uhaba wa wahadhiri nchini. Rai hiyo ameitoa Ikulu Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kutunuku Hati Idhini kwa vyuo vikuu nane ambavyo vimekamilisha taratibu zote za uanzishwaji wa vyuo.

Alisema Tanzania ina upungufu mkubwa wa wahadhiri wenye sifa za kufundisha vyuo vikuu, jambo ambalo linachangia baadhi yao kufundisha zaidi ya chuo kimoja.

“Nasikia Maprofesa hawatoi fursa za watu kusoma Masters na Phd, programu hizi mzipanue, msitoe fursa kidogo, wekeni malengo ili kila mwaka mzalishe walimu.

“Tusipofanya hili hatutapata wasomi wa kutosha, kwa sababu hii ndiyo njia ya kupika wasomi, tuondoe ile dhana ya kuibiana wahadhiri, wakati mwingine unakuta mhadhiri mmoja anafundisha vyuo zaidi ya vitatu, hii si sawa lipeni uzito jambo hili,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo, aliwataka wamiliki na wakuu wa vyuo kuhakikisha wanatoa elimu iliyo bora ili vijana wanaohitimu waweze kukubalika katika soko la kimataifa.

Rais Kikwete pia aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, kusimamia mpango wa matokeo ya haraka (big result now), ili kukidhi idadi ya ongezeko la vyuo.

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha inatoa wahitimu 80,000 kwa mwaka, tofauti na sasa ambapo ni wanahitimu 40,000.

Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Profesa Tolly Mbwete, alisema anakubaliana na wito wa Rais Kikwete kuhusu uhaba wa wahadhiri kwa sababu hali ni mbaya sana.

“Kwa muda mrefu jambo hili lilikuwa halijawekewa uzito unaostahili, ni wajibu wa vyuo hasa vile vya umma kukutana na kupangiana majukumu tusipofanya hivi mchezo wa kuibiana wahadhiri hautakoma,” alisema Profesa Mbwete.

Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Titus Mdoe, alisema wamekuwa wakiwatumia wahitimu wa Shahada ya kwanza waliofaulu vizuri ambao huwaongezea mafunzo ya ziada na kuwaendeleza.

Kutunukiwa kwa Hati hizo, kunakamilisha idadi ya Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu vishiriki nchini kufikia 50, ambapo kwa pamoja vitatoa nafasi 78,735, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu. Kila mwaka wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu ni 43,116. 

Vyuo vilivyoidhinishwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (TUMA), Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (RUCo), Maunt Meru (MMU), Arusha (UoA) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini (TUDACo).

Vingine ni Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha (NM-AIST) na Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).


Chanzo:http://www.mtanzania.co.tz
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment