Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, August 13, 2013

MALI: CISSE AMPONGEZA BOUBACAR KEITA

Ibrahim Boubacar keita
                                            Ibrahim Boubacar keita
Mgomboea urais nchini Mali Soumalia Cisse amekubali kushindwa na mpinzani wake Ibrahim Boubacar Keita katika duru ya pili ya uchaguzi  uliofanyika Jumapili. Akizungumza Jumatatu  jioni Cisse alisema bw. Keita alishinda uchaguzi huo kwa njia halali na kumtakia kila la kheri.

Msemaji wa bw.Keita, Mamadou Camara alisema matokeo yanaonyesha kuwa alipata kati ya asili mia 70 na 80 ya kura.Camara alisema bw. Cisse alimtembelea Keita nyumbani kwake  Jumatatu jioni na kumpongeza kufuatia ushindi huo.

Akizungumza na  idhaa ya Kifaransa ya Sauti ya Amerika Jumanne  msemaji huyo  alisema kuwa ushindi wa bw. Keita  ulikuwa mkubwa na kwamba sasa ataelekeza nguvu zake zote katika kuleta maridhiano ya kitaifa nchini Mali.


Imewkwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment