Writen by
sadataley
7:29 PM
-
0
Comments
KANISA LA KIINJILI
LA KILUTHERI TANZANIA
DAYOSISI YA
IRINGA
NAFASI YA KIJANA KATIKA
KANISA.
SOMO LILOTOLEWA
KATIKA KONGAMANO LA VIJANA KATIKA USHARIKA WA KIHESA
29-06-2013
- KANISA NI NINI?Kanisa si jengo tu bali ni wale waliomo ndani yake. Maana yake ya asili toka neno la Kiyunani ni ekklesia “kusanyiko” walioitwa kama maneno katika msalaba ambao huwa ninauvaa. Neno Kanisa Iimo katika Biblia, Matendo ya mitume 17:24 "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono."
Kanisa ni watu wanao amini Waefeso
2:21 "Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe
hekalu takatifu katika bwana." 1Wakorintho 3:16 "Hamjui ya kuwa ninyi
mmekuwa hekalu la Mungu na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?.
Kazi ya kanisa ni ipi? Kanisa linaeneza
ijili 2 Timotheo 4:2 "Lihubiri neno
uwe tayari wakati ufaao na wakati usiokufaa karipia kemea na kuonya kwa
uvumilivu wote na mafundisho."
Kanisa limepewa maagizo na Mungu
Waefeso 4:12 "Kwa kusudi kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma
itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe."
Kila mshiriki ana jukumu maalum 1
Wakorintho 12:13, "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa
mwili mmoja kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani ikawa tu watumwa au ukawa
tu huru nasi tulinyweshwa Roho mmoja."
Wakristo tu wafariji wenzetu Waebrania
10:25 "Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine;
bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa
inakaribia.
B. KIJANA NANI
1.
Ujana
ni hatua ambayo mtu anaipitia baada ya utoto au ni kipindi cha kati cha makuzi
ya mtu kabla ya utu uzima na hatimae uzee
2.
Ujana
huanza mara baada ya mtu kubadilika kimaubile na huanzia miaka kumi na mbili
wengine hadi kumi na tano ambapo mtu huanza kuwa na hisia za kimwili na
kutamani sana kuwa na uhuru wake katika maamuzi. Mabadiliko haya huchochea au
hupelekea hisia mbalimbali za kimwili na mabadiliko ya jumla ya tabia
3.
Ujana
ni majira yanayopita katika makuzi ya mwanadu, ukifanikiwa kuwa mzee ni lazima
ulipita katika kipindi hiki au daraja hili la ujana, kwa hiyo kama bado uko
katika dara hili ni muhimu kujipanga ili usije ukajilaumu mbele ya safari
UMRI
WA KIJANA KIKANISA
Kanisa linamtambua kijana baada ya
kupata kipaimara wengi hupata kuanzia miaka kumi na miwil-kumi nan ne na ukomo
wa ujana ni miaka arobaini na tano (12-45)
Hivyo napenda kusema kuwa ndiyo sababu siku zote
nikijitazama kama kijana humuona Mungu kuwa ni wa ajabu kuniumba hata mimi na
kunifanya kuwa Mchungaji. Hivyo hukubaliana na nyimbo na waimbaji hawa ambao
wamewahi sema kupitia nyimbo zao kuwa
a.
“Mungu wetu ndiye Boma”- Tumwabudu Mungu Wetu 302 na Dr.
Martin Luther
Mungu ndiye ngao yetu na siraha yetu shetani akija kwetu
tukiwa naye daima tutashinda na maadui zetu (shida,adha na changamoto za maisha
yetu yote). Tumtazame yeye kama Dr.
Martin Luther alivyosema katika maneno ya wimbo wake huu. Anaimba wakati akiwa
katikati ya mapambano na sisi tuimbe tunapopita katika hali mbalimbali katika
maisha yetu.
b.
“Mungu ni Mwaminifu”. -Solomon Mkubwa
Mungu hatotuacha daima yeye hutunza maagano(makubaliano yetu
nay eye) hivyo hata sisi tulivyo hapa anatujua na anaendelea kutunza uaminifu
wake kwetu hivyo na sisi tusimame kwake tu, tumtazame yeye pekee.
c.
“Liseme kwani ni jambo usilolijua”- Sarah K
kwani ni hakika hatuna tunalolijua katika
maisha yetu ni yeye (Yesu) anatuwezesha ,ametuwezesha na ataendelea kutuwezesha.
d.
“I will be There, Just Call My
name”. -Michael
Jackson&Mariah Carey
Ipo siku tutaitwa kwenda Mbinguni na kila mmoja wetu ataitwa
kwa jina lake; hivyo tujiandae.
e.
“Heri Kumjua Yesu Bwana”. Tumwabudu Mungu Wetu 175 na F.J Crosby
Ni Yesu pekee atatuwezesha na kutuvusha na hata sasa anajua
tulikotoka,tulipo na tuendako.
f.
“Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana”.
Tumwabudu Mungu Wetu 268 na samuel
Stone
Kama tulivyoimba siku ile ya Kipaimara hebu tuendele
kumtazama yesu kama msingi wa Kanisa na ndiyo njia pekee ya kutuvusha vijana,
njooni tumtumikie kadili ya nafasi tunazojali. Tusiogope huku ni kuzuri tu
hakuna shida yoyote.
KIJANA KAMA
- MSHARIKA
MKAMILIFU ALIYEPO NA AJAYE
- KIONGOZI
WA KANISA-MZEE WA KANISA-MTUMISHI WA MUNGU KATIKA KADA MBALIMBALI
- MLEZI
WA FAMILIA AJAYE NA ALIYEPO (wajibu wako pale nyumbani kwa sasa).
- MZAZI
AJAYE – (unayoyafanya sasa nawe
utafanyiwa na m/watoto wako).
- MTETEZI
WA WANYONGE (Haki za wanyonge na
wanaonyanyaswa kuto kaa kimya kwani Dr. Martin Luther alisema utawajibika
kwa yale uliyoyasema na usiyoyasema lakini ulipaswa kuyasema na umekaa
kimya.)
- MWANA
MAENDELEO ( Jiandae kuajili au
kuleta mabadiliko katika eneo ambalo Mungu atakupa/amekupa).
A. “Mkumbuke Muumba wako siku za
ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya…” (Mhubiri12:1)
B. “Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu,
na neno la Mungu linakaa ndani yenu,
nanyi mmemshinda yule mwovu”.
(I Yohana 2:14b).
C. “Na nimwibie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu
katika habari za shamba lake la mzabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la
mizabibu,kilimani penye kuzaa sana;akafanya handaki kulizunguka pande zote,
akatwaa mawe yake,akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, akajenga mnara
katikati yake, akachimba shinikizo ndani yake;akatumaini ya kuwa utazaa zabibu,
nao ukazaa zabibu-mwitu. Na sasa, enyi wenyeji wa yerusalem, namyi watu wa Yuda
amueni, nawasihi mkato, kati ya mimi na shamba
langu la mizabibu….”(Isaya 5:1-7).
MAMBO YA KUZINGATIA NI:-
“Huwezi kuyajali maisha yako kama
hujui thamani yake, huwezi kujua thamani ya maisha yako kama hujajitambua kwa
Neno la Mungu, huwezi kuwa na maisha ya mafanikio kama maamuzi yako
hayatengenezi mafanikio, ufahamu sahihi juu ya maisha yako ndio msingi wa
kujitambua kwako, yaani kuijua Kweli ili hiyo Kweli ikuweke huru na ndipo
utakapokuwa huru kweli kweli, kumbuka hata usipoamua maisha yako yataendelea
kama kawaida. Zaidi ya hayo kama hujui wewe ni nani huwezi kujua thamani yako,
kama hujui thamani yako lazima utaishi chini ya kiwango cha maisha unayotakiwa
kuishi”.
UTAIJUAJE NAFASI YAKO KAMA KIJANA
Nafasi yako kama Kijana ni wajibu
wako, umuhimu ulionao kwako na kwa jamii kwa ujumla wake pamoja na familia
yako. Lazima ujue nafasi yako katika maeneo yafuatayo:
• Kwako binafsi,
• Katika familia yako,
• Kwa Kanisa lako,
• Kwa jamii yako
• kwa mkoa wako,
• kwa Taifa lako na
• kwa Ufalme wa Mungu.
Safari ya kujua nafasi yako katika
maeneo yako hayo hayo hapo juu inaanzia katika eneo moja tu ambalo ni KUJITAMBUA
KUJITAMBUA NI NINI
“Kujitambua ni hali ya kuwa na
ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na
mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au
kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana
na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na
nguvu ya taarifa unazopata.
HIVYO BASI KIJANA ANATAKIWA
KUJUA KUWA:-
1. Kujitambua ni hatua ya muhimu
katika maisha ya mtu yoyote duniani kama anataka kuishi kwa Furaha na matumaini
na kufikia malengo yake
2. Kujitambua ni matokeo ya kupata
ufahamu sahihi juu eneo fulani utakaokusaidia kufanya maamuzi sahihi katika
eneo husika ili uweze kufanikiwa
3. Ufahamu au maarifa unapatikana
kwa kutafuta, kuchunguza na kudadisi taarifa mbalimbali kwani si kila namna ya
kujitambua ni sahihi kwa kijana
4. Matokeo ya ufahamu ulionao
yatafanana na ubora wa maisha unayoishi kwa kiwango cha kuathiri maamuzi yako
ya kila siku
5. Kiwango cha matokeo ya kujitambua
kitafanana na ubora wa taarifa ulizozipata
6. Udhihirisho wa maisha ya
kujitambau ni hatua ya juu kabisa ya kuthibitisha kwamba kweli umejitambua.
KWANINI KUJITAMBUA NI LAZIMA:-
1. Ni lazima ujitambue, upate
ufahamu sahihi juu ya maisha yako pamoja na mambo yote na jamii inayokuzunguka
2. Ni muhimu ujue wajibu ulionao
kwako wewe mwenyewe kama mtu binafsi juu ya maisha yako
3. Kuna haja ya kujua kuwa wewe ni
sehemu ya familia yako na lazima ujue wajibu wako kwa wazazi na familia kwa
ujumla
4. Ni lazima ujifunze kuwa mzalendo
wa taifa lako sawa na jinsi ambavyo Mungu anataka, fahamu kuwa umeunganishwa na
ardhi ya Tanzania kwa mafanikio yako, Mungu akikwambia nenda nje ya nchi nenda
lakini usifikiri mafanikio hayako Tanzania
5. Kijana anatakiwa ajitambue,
ajielewe yeye ni nani na ana kusudi gani katika maisha yake
6. Unatakiwa kupata uelewa wa
kutosha juu ya kipindi cha ujana na umuhimu wake ukiwa bado Kijana ili ujue
namna ya kuzingatia na kujipanga kwa hapo baadae
7. Kuelewa changamoto zilizopo
katika kipindi cha ujana na namna ya kuzishinda kuna uhusiano na namna
unavyojitambua ukiwa bado kijana
8. Kujenga shauku, nia na kiu kwa
kijana ili aweze kuishi maisha yenye mwelekeo na aweze kutimiza maono yake
akiwasaidia na wengine kumjua Mungu na maisha yake kwa ujumla wake
9. Kuwekeza uthamani na nguvu ya
kipindi cha ujana kwa mtazamo wa Ufalme wa Mungu.
KIJANA MWENZANGU CHUKUA MUDA
KUTAFAKARI MISTARI HII
Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. - Yohana 3:16
kwa
sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; -
Warumi 3:23
Kwa
maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
katika Kristo Yesu Bwana wetu. - Warumi 6:23
Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi. - Yohana 14:6
Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake; - Yohana 1:12
Yesu
akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili,
hawezi kuuona ufalme wa Mungu. - Yohana 3:3
Na
katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu
hakuna ondoleo. - Waebrania 9:22
akasema,
Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika
ufalme wa mbinguni. - Mathayo 18:3
Tazama,
nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango,
nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. - Ufunuo wa Yohana 3:20
Tukiziungama
dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na
kutusafisha na udhalimu wote. - I Yohana 1:9
Kwa
sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni
mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu
huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. kwa kuwa,
Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. - Warumi 10:9,10,13
Kwa
maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi
zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
- Waefeso 2:8,9
si
kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa
kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; - Tito 3:5
Wakamwambia,
Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. - Matendo ya Mitume 16:31
Amwaminiye
Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya
Mungu inamkalia. Yohana 3:36
Nami
nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu
atakayewapokonya katika mkono wangu. - Yohana 10:28
Hata
imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita
tazama! Yamekuwa mapya. - II Wakorintho
5:17
Imeandaliwa na
Mchg Kurwa Sadataley- Mratibu wa
Idara
Habari na Mawasiliano KKKT-DIRA
No comments
Post a Comment