Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Wednesday, June 7, 2017

UN yaipa DRC siku 2 ichunguze mauaji na jinai eneo la Kasai

Miili iliyofukuliwa kwenye kaburi la umati eneo la Kasai, miezi 2 iliyopita
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameipa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku mbili ionyeshe azma na irada ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji na jinai za kibinadamu katika eneo la Kasai.
Zeid Ra'ad al-Hussein amesema iwapo hatapokea ripoti ya pamoja ya asasi za serikali ya DRC kuhusu uchunguzi wa jinai hizo kufikia Juni 8, basi atasisitizia udharura wa kuundwa mchakato wa kimataifa wa kuchunguza mauaji hayo. 
Al-Hussein ameyasema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva na kuongeza kuwa, lazima uchunguzi ufanyike kuhusu jinai za kibinadamu katika eneo la Kasai, hususan baada ya makaburi kadhaa ya umati kuguduliwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 400 wameuawa huku wengine zaidi ya milioni 1.2 wakilazimika kuyahama makazi yao tangu machafuko na mapigano yashadidi katika eneo hilo.
Hii ni katika hali ambayo, mahakama moja Kongo DR imeanza kuchunguza faili la mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa yaliyojiri katika mkoa wa Kasai mwezi Machi mwaka huu.
Eneo la Kasai la katikati mwa Kongo DR limekuwa likishuhudia mapigano makali baina ya wanamgambo wa kikabila na askari wa serikali tangu mwaka jana 2016. 
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment