Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Saturday, June 10, 2017

Umoja wa Ulaya wakosoa kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

Umoja wa Ulaya umekosoa mwenendo wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika maeneo ya Wapalestina.
Gazeti la al-Quds al-Arabi limeunukuu Umoja wa Ulaya ukitangaza kuwa, kuendelea sera za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina ndiko kunakoitatiza zaidi kadhia ya Palestina.
Sambamba na kukosoa mwenendo huo, Umoja wa Ulaya umesisitiza kwamba, ukishirikiana na weashirika wake wa kieneo na kimataifa uko tayari kuunga mkono juhudi za kufikiwa ufumbuzi wa kadhia ya Palestina kwa njia za amani.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel ulipasisha mpango wa ujenzi wa nyumba mpya 1500 katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, uamuzi ambao unaendelea kukosolewa ndani na nje ya Palestina.

Ujenzi wa vitongoji hivyo, unaendelea katika hali ambayo, Disemba mwaka jana, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio linalotaka kuhitimishwa ujenzi wa vitongoji hivyo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Aidha maafisa mbalimbali wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kieneo na kimataifa ya kutetetea haki za binadamu wamekuwa wakisisitiza kwamba, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ujenzi wa vitongoji unaofanywa na Israel katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina ni kinyume cha sheria na inapaswa usimamishwe kikamilifu.
Parstoday
Pa

  • « PREV
    NEXT »

    No comments

    Post a Comment