Writen by
sadataley
10:54 AM
-
0
Comments
MASHINDANO ya kombe la Ritta Kabati Challenge Cup 2017 jumamosi hii yanaingia hatua ya mznguko wa kwanza huku timu za Mshindo Fc na Polisi Iringa wakionyesha kutambiana kwa kila mmoja kumfunga mwenzake .
Uongozi wa timu ya Mshindo umesema kuwa unauhakika wa kuwalaza mahabusu kwa kuwagagadua kama si kuwafunga kwa jumla ya magoli yasiyopungua matatu timu ya polisi Iringa ambayo tayari ilikwisha fungwa goli 3 -0 katika mchezo wao wa kirafiki .
Kuwa timu hiyo ya Mshindo ambayo inajivunia kwa kutokusajili zaidi ya wachezaji kujipeleka kutaka kuichezea timu hiyo ,kuwa wapo vizuri kutoa upinzani mkubwa kwa timu ya polisi na ikiwezekana ubingwa wa mashindano hayo ubaki Mshindo FC .
Joel Msiba ni msemaji wa timu ya polisi Iringa alisema kuwa timu yake imejipanga vema kuifunga timu ya Mshindo FC katika mchezo wao huo utakaopigwa siku ya jumamosi huku akiomba mashabiki zaidi kujitokeza kushuhudia mchezo huo .
Msiba alisema kwa kawaida timu ya polisi ni timu ya wastarabu ambao wapo kuona michezo ndani ya mkoa wa Iringa inahamasishwa na kupitia mashindano hayo kuhakikisha timu yake haishiriki tu bali inatwaa ubingwa wa mashindano hayo .
Kuanzishwa kwa mashindano hayo ya hayo ya kombe la mbunge Ritta Kabati kumeendelea kuhamasisha vijana wengi kushiriki katika michezo hiyo ambayo ilianza kwa kuwa na timu zaidi ya 42 na kufanya mashindano hayo kuwa moja kati ya mashindano makubwa zaidi kwa kushirikisha timu nyingi ukilinganisha na ligi kuu ya VPL .
Chanzo: Matukio daima
No comments
Post a Comment