Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Saturday, June 10, 2017

Kassim Majaliwa: Polisi, Uchukuzi na Maji kunanuka Rushwa




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maeneo mabayo bado yana tatizo la Rushwa ni  pamoja na Sekta ya Uchukuzi, Jeshi la Polisi na Idara za Maji,

Majaliwa amesema hayo jana wakati akifungua mafyunzo ya mbili kwa wabunge wa kamati ya Kupambana na Rushwa (APNAC)

amesema kuwa rushwa bado ni ugonjwa unaoisumbua  nchi kwa kiasi kikubwa na kufanya mambo mengine yaendelee kutiliwa mashaka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na watawala.


Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa African Dream chini ya ufadhiri wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, (UNDP) kwa lengo la kuwajengea uwezo wabunge ili kupambana na tatizo hilo ambalo linaendelea kuwa mwiba mchungu kwa serikali.

Majawali amesema kwa sasa serikali imeamua kwa makusudi mazima kupambana na tatizo hilo na inafanya hivyo kwa kujua bado mchango wa taasisi nyingine unahitaji kumaliza jambo hilo.



Hata hivyo amesema mkakati wa serikali ni pamoja na kuziomba mamlaka zinazohusika ikiwammo mahakama kuendesha kesi zote zinazohusiana na rushwa kwa haraka zaidi na kutoa hukumu ili pale inapobidi wahusika wachukuliwe hatua stahiki.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, serikali imeokoa kiasi cha Sh 53.9 bilioni tangu kuanza rasmi kwa mkakati wa mapambano hayo 2015/16 na wanaendelea kufanya mkakati wa kuzuia siyo kukamata.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment