Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, November 1, 2016

China yaonesha hadharani ndege mpya za kivita.

Two J-20 jets at Zhuhai airshow

Image copyrightREUTERS
China imeonesha hadharani ndege zake mpya za kivita aina ya J-20 ambazo zina uwezo wa kujificha kwenye zisionekane kwenye mitambo ya rada.
Ndege mbili za aina hiyo zilipaa angani kwa sekunde 60 wakati wa maonesho ya ndege ya Zhuhai katika mkoa wa Guangdong.
Maonesho hayo huwa makubwa zaidi nchini humo na huwakutanisha waundaji na wanunuzi wa ndege.
Ndege hizo zinatazamwa na wengi kama ishara ya hamu ya Beijing kuboresha na kuimarisha uwezo wake kijeshi.
Rais wa China Xi Jinping anataka kuimarisha majeshi ya nchi yake huku taifa hilo likiendelea kudhihirisha ubabe sana kuhusu umiliki wa maeneo ya bahari Kusini na Mashariki mwa China.
Ndege ya kivita ya J-20 maonesho ya ZhuhaiImage copyrightREUTERS
Image captionNdege ya kivita ya J-20 maonesho ya Zhuhai
Ndege hizo za J-20 zimeundwa na kampuni ya Chengdu Aircraft Industries Group, ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la ndege la China ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Aviation Industry Corporation of China.
Baadhi wamelinganisha ndege hizo na ndege aina ya F-22 Raptor za Lockheed Martin.
Mchanganuzi wa masuala ya ndege Bradley Perret amesema ndege hiyo "bila shaka ni hatua kubwa katika uwezo wa kivita wa China".
ZhuhaiImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionNdege ya kusafirisha mizigo ya Y-20 pia imezinduliwa katika maonesho hayo ya Zhuhai
Ndege ya kwanza kabisa ya kubeba mizigo mizito ambayo imetengenezewa nchini China, ndege ya Y-20, pia imezinduliwa katika maonesho hayo.
Ndyingine zinazotarajiwa ni ndege kubwa ya AG-600 ya kusaidia katika uokoaji na kushika doria baharini.
Aidha, ndege ya kivita ya kuangusha mabomu kwa jina Xian H-6K na helikopta ya kutekeleza mashambulizi ya Changhe Z-10K zitazinduliwa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment