Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Monday, November 7, 2016

BURIANI SAMWEL SITTA

Ndugu zangu,
Watanzania zimetufikia habari alfajiri ya leo, kuwa ndugu yetu , Mzee Samwel Sitta, Spika Mstaafu na aliyepata kuwa Mbunge wa Urambo, amefariki dunia.
Atakumbukwa kwa mengi, moja kubwa kwenye mchango wake kwenye kupata Katiba Mpya. Atakumbukwa kwa kutetea maslahi ya Watanzania.
Na hapa tutaikumbuka kauli yake ya kijasiri pale alipotamka hadharani kupinga uonevu wa kampuni ya Dowans kwa Watanzania kufuatia sakata lile la Dowans kutaka kulipwa mabilioni ya shilingi kufuatia mkataba tata.
Samwel Sitta alitamka;
" Dowans wanatuchezea mchezo wa kwenye makaratasi ili wajipatie mabilioni ya shilingi za Watanzania. Uamuzi wa kuwalipa hao Dowans haukufikiwa na Baraza la Mawaziri. "- Samwel Sitta.
Buriani Samwel Sitta.
habari kwa mtandao wa Mjengwa Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment