Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, October 14, 2016

Mfalme wa Thailand Bhumibol kuombolezwa mwaka mmoja

Watu walia kuomboleza Mfalme Bhumibol Adulyadej Bangkok, Thailand, Alhamisi 13 Oktoba 2016.

Image copyrightAP
Image captionWatu wengi waliokuwa nje ya hospitali alimokuwa amelazwa Mfalme Bhumibol walilia kwa huzuni baada ya kifo chake kutangazwa

Raia wa Thailand wameanza kuomboleza kufuatia kifo cha Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye alikuwa nguzo ya uthabiti wa kisiasa nchini humo wakati wa utawala wake uliodumu miaka 70.
Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye ndiye mfalme aliyetawala muda mrefu zaidi duniani, alifariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 88.
Umati mkubwa wa waombolezai walikesha Bangkok wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeusi, na wengi sasa wanarejea katika barabara za mji.
Mwili wa mfalme huyo utapelekwa katika hekalu la Temple baadaye leo.
Maombolezi rasmi yatadumu kwa mwaka mmoja.
Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kwa mfalme mpya, lakini ameomba shughuli yake kurithi madaraka icheleweshwe kidogo.

Maelfu wamejitokeza barabara za Bangkok kusubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo 14 Oktoba 2016
Image captionMaelfu wamejitokeza barabara za Bangkok kusubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo
Waombolezaji barabarani (14 Okt 2016)Image copyrightAP
Image captionRaia wa Thailand ambao walimchukulia mfalme huyo kuwa nguzo ya uthabiti wamesikitishwa na kifo chake.

Baraza la mawaziri lilitangaza siku ya Ijumaa kuwa siku ya mapumziko.
Bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kwa siku 30 zijazo.
Serikali imewaomba watu wavalie mavazi ya rangi nyeusi na kujiepusha na hafla za "furaha" kipindi hicho.
Tovuti za habari nchini humo zimegeuza rangi za kurasa zake kuwa za rangi nyeusi na nyeupe.
Viongozi mbalimbali duniani wamekuwa wakituma salamu za rambirambi.
Maelfu ya waombolezaji wamefika katika barabara za mji wa Bangkok wakisubiri msafara wa kusafirisha mwili wa mfalme huyo kutoka hospitali ya Siriraj hadi Kasri Kuu Ijumaa adhuhuri.
Mwanamfalme anayetarajiwa kuwa mrithi wa ufalme ataongoza shughuli za kuosha maiti ya mfalme huyo, tambiko la Kibuddha, Ijumaa jioni, maafisa wa kasri wamesema.

Bangkok 14 Oktoba 2016
Image captionWengi wanavalia mavazi ya rangi nyeusi Bangkok
Mfalme Bhumibol AdulyadejImage copyrightEPA
Image captionMamia ya watu wamejitokeza kuomboleza nje ya kasri la Grand Palace, Bangkok
Bangkok (14 Okt 2016)Image copyrightREUTERS
Image captionMfalme huyo alipendwa sana na raia wa Thailand ambao walimchukulia kama mteule wa Mungu

Mfalme Bhumibol alichukuliwa kama nguzo ya uthabiti kwenye taifa hilo lililokumbwa na misukosuko ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.

Mfalme Bhumibol AdulyadejImage copyrightEPA
Image captionWengi waliomboleza hadharani baada ya habari za kifo chake kutangazwa

Thailand bado inatawaliwa na jeshi ambalo lilitwaa mamlaka kupitia mapinduzi 2014. 
Mwanamfalme Maha Vajiralongkorn anatarajiwa kuwa mfalme mpya, amesema tangazo hilo litatolewa baadaye.
Amethibitisha kwamba atatekeleza majukumu yote kama mfalme mtarajiwa, lakini akawataka raia waomboleze kifo cha babake kwanza. 

Maha VajiralongkornImage copyrightAFP
Image captionMwanamfalme Vajiralongkorn hajafahamika sana na raia wa Thailand

Mwanamfalme Vajiralongkorn, 64 hajafahamika sana na raia wa Thailand na hajapendwa sana na raia kama babake.
Ameishi muda mwingi nje ya nchi, sana Ujerumani.


« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment