Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, June 29, 2015

Uchaguzi wa ubunge wafanyika Burundi

Uchaguzi wa ubunge unaendelea nchini Burundi licha ya wiki ya maandamano ya ghasia dhidi ya uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kuwania muhula wa tatu. Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuchelewa baada ya maguruneti kurushwa. Upinzani umesusia uchaguzi huo.Muungano wa Ulaya unasema kuwa uchaguzi huo utazidisha mgogoro uliopo. Umoja wa Afrika umekataa kutoa waangalizi ukisema kuwa baadhi ya masharti yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki. Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze.Karibu watu 130,000 wamelitoroka taifa hilo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment