Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, June 4, 2015

Kofi Annan amtaka Nkurunziza kujiuzulu

Aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan amemtaka rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kujiuzulu huku uchaguzi mkuu ukiahirishwa. Kumekuwa na maandamano ya ghasia nchini Burundi pamoja na mapinduzi yaliofeli tangu Nkurunziza atangaze kuwa atawania muhula mwengine wa tatu wa urais katika kile watu wanaamni ni ukiukaji wa katiba. Annan ameiambia BBC kwamba rais huyo amepoteza uhalali wake na sasa anafaa kujiuzulu iwapo anawajali raia wa Burundi. Matamshi hayo ya Annan yataongeza shinikizo kwa rais Nkurunziza ,ambaye hadi sasa hajatoa ishara zozote za kujiuzulu. Uchaguzi wa bunge pamoja na ule wa urais umehairishwa kufuatia wiki za maandamano ya ghasia. Viongozi wa jumuia ya Afrika Mashariki walipendekeza uchaguzi wa bunge na urais uahirishwe kwa wiki sita kufuatia ghasia za kumpinga rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Uchaguzi wa Rais unatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment