Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 1, 2015

Maandamano mapya Baltimore Marekani

Kumetokea maandamano mapya nchini Marekani katika mji wa Baltimore kufuatia kifo cha kijana mweusi Freddie Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi. Mamia ya watu wameandamana katika mitaa, wakionyesha ujasiri licha ya hali mbaya ya hewa iliyokuwepo. Matokeo ya mwanzo ya uchunguzi wa polisi wa jinsi kijana wa miaka ishirini na mitano mwenye asili ya weusi alivyouawa bado hayajawekwa hadharani. Mtetezi wa haki za binadamu, Mchungaji Al Sharpton, ameitisha mkutano mjini Baltimore ili kuimarisha uhusiano baina ya polisi na wanajamii.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment