Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, April 15, 2015

Drogba arejesha alichojaaliwa kwa jamii.

Mshambuliaji wa timu ya Chelsea F.C. Didier Drogba amezindua hospitali ya kwanza, kubwa na ya aina yake kati ya tano alizo wahi kuahidi kuzijenga kama sehemu ya kujitolea kwa jamii yake . Hospitali hiyo iko wilaya ya Attécoubé katika mji wa kibiashara wa Abidjan, hospitali hiyo imemgharimu nguli huyo wa kandanda kiasi cha dola milioni moja za kimarekani ili kukamilisha mjengo huo wa afya ;na hospitali hiyo ni maalumu kwa wanawake na watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu . Hospitali hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba mia nane (800) huduma kadhaa zinapatikana ikiwamo chumba cha uchunguzi, wodi ya wazazi,kitengo cha watoto,jengo la x-ray ,jengo la kisasa la maabara,duka kubwa la dawa,jengo la kulaza wagonjwa na jengo tengefu la wagonjwa. Inakadiriwa hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu hamsini kwa mwaka na hii ni kwa muujibu wa katibu mkuu wa asasi ya Didier Drogba Foundation , Guy Roland Tanoh ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo. Hospitali zingine nne zilizo katika ahadi za mwanasoka huyo ziko katika hatua za ujenzi za mwisho mwisho kukamilika ambazo ziko nchini Ivory Coast katika miji ya Yamoussoukro, San Pedro, Man na Korhogo na zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao. Asasi hiyo ya Drogba foundation inaandaa chakula cha hisani mjini London mwezi huu wa April tarehe 18 ili kupata fedha za kukamilisha miradi hiyo. Mshambuliaji huyo wa timu ya Chelsea na pia timu ya Elephants anabakia kuwa mchezaji na mfungaji bora na wa mfano wa kuigwa nchini mwake pamoja na kwamba amestaafu kuichezea timu yake ya taifa,ambayo iliutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa mwaka huu nchini Equatorial Guinea mnamo mwezi wa February. Kazi nzuri Didier Drogba! .
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment