Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 29, 2015

Kesi ya Mtikila vs Mahakama ya Kadhi kusikilizwa Machi 30 yapangiwa Jaji .

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Machi 30, mwaka huu kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila, akipinga kitendo cha Serikali kupeleka Muswada bungeni wa kutunga sheria ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, kwamba uko kinyume na Katiba ya nchi. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Richard Mziray. Katika kesi hiyo kupitia hati yake ya madai iliyopewa usajili namba 14 ya mwaka huu, Mtikila: 1.Ameiomba mahakama itoe amri kwamba wale walio kwenye mamlaka ya Serikali akiwaemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Mary Nagu; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira na wenzao watoe sababu kwa nini wasifungwe kifungo kisichopungua miaka mitano endapo watashindwa kujieleza. 2.Itoe amri ya vigogo hao kufungwa kifungo hicho kutokana na kuchezea Katiba ambayo ni sheria mama ya nchi. 3.Ameiomba mahakama itoe amri kwamba Mahakama ya Kadhi na Jumuia ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC) itangaze ni haramu kwenye ardhi ya Tanzania. 4.Anadai kuwa suala la serikali kuandaa muswada wa Kiislamu na kuuwasilisha bungeni na kitendo cha Bunge kukubali ni sawa na uhaini. Anadai kuwa kitendo hicho ni sawa na uvunjifu mkubwa wa viapo walivyoapa viongozi hao wakati wa kushika madaraka ya umma na ni kinyume cha ibara ya 19 ya katiba ya nchi inayoeleza kwamba masuala ya dini na kuabudu yatakuwa ni ya mtu binafsi na kwamba uendeshaji wa mambo au taasisi za kidini hazitakuwa sehemu ya mamlaka ya nchi. Chanzo: http://www.wavuti.com/2015/03/kesi-ya-mtikila-vs-mahakama-ya-kadhi.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment