Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 31, 2015

Buhari aongoza katika matokeo ya awali Nigeria

Matokeo ya awali ya kura zilizopigwa siku ya jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan. Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos. Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao. Huku zaidi ya nusu ya matokeo yakiwa yametangazwa mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari yuko mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan. Hata hivyo matokeo bado hayawezi kutabiriwa kwa kuwa majimbo yenye watu wengi kama Lagos na Rivers hayajatangaza matokeo yake. Mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali. Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment