Writen by
sadataley
2:00 PM
-
0
Comments
Rais wa Tanzania, Jakaya KikweteRais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala cha Mapinduzi (CCM), amesema kwamba mgombea Urais wa chama chake bado hajajitokeza hadharani.
Rais Kikwete alisema hayo katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, na kuzua mjadala kutokana kwamba kuna wanachama waliojitokeza na kuonyesha nia ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba.
Kufuatia kauli hiyo, Idd Ligongo wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, aliongea na Profesa Mwesiga Baregu, wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, ili kupata uchambuzi juu ya kauli hiyo.
No comments
Post a Comment