Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, January 29, 2015

CILT WAANDAA MKUTANO MKUBWA ARUSHA,MWAKYEMBE AUBARIKI.


Aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni aziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizungumza na wadau mbalimbali walojitikeza katika afla hiyo ya kutafuta fedha za kuendesha mkutano huo utakao fanyika mapema mwezi wa tatu.
Taasisi ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi wa bidhaa CILT yani THE CHARTERD INSTITUTE OF LOGISTIC AND TRANSPORT Tawi la Tanzania imeandaa mkutano mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa arusha tarehe 3 na 4 mwezi wa tatu mkutano wenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli katika secta hiyo.

Mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE akizungumza kuhusu mkutano huo na taasisi hiyo inavyofanya kazi. Mkutano huo ambao utafanyika katika hoteli ya mount meru jijini arusha una mipango pia ya kuwakutanisha wanataaluma wa maswala ya uchukuzi na usafirishaji wa bidhaa ili kubadilishana uzoefu katika taluma hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupata chai yenye lengo la kuchangisha fedha ambazo zitasaidia katika kuendesha mutano huo aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikian wa Africa mashariki MH HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kama huu ni fursa ya kipekee ambayo nchi inatakiwa kujivunia na kuitumia kujitangaza kimataifa.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza. Amesema kuwa mkutano huo utawasaidia hasa vijana ambao wanasoma maswala haya kukutana na wazoefu katika fani hiyo na kubadilishana uzoefu jambo ambalo litawajengea uzoefu katika kazi zao pindi watakapoingia katika fani.
Chanzo: MJENGWA  BLOG
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment