Writen by
sadataley
4:47 PM
-
0
Comments
Buriani kwa Rais Michael Sata Zambia

Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na umri wa miaka 77.Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa umelazwa katika majengo ya bunge.

Rais Sata atazikwa katika eneo lenye makaburi yaliyotengewa Marais wa nchi hiyo.
Taifa hilo kwa sasa linaongozwa na kaimu Rais huku uchaguzi mkuu ukipangwa kufanyika katika muda wa miezi michache ijayo.
No comments
Post a Comment