Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Friday, October 10, 2014

Ufaransa: Patrick Modiano ashinda tuzo la Nobel
Patrick Modiano, ashinda tuzo la Nobel mwaka 2014.
Patrick Modiano, ashinda tuzo la Nobel mwaka 2014.

         
Patrick Modiano, raia wa Ufaransa, ameshinda taji la Mwandishi bora wa tuzo la Nobel mwaka 2014


Modiano mwenye umri wa miaka 69, ameshinda tuzo hiyo kutokana na kazi yake ya uandishi kuhusu vita vya pili vya dunia, na kuhusu maisha ya binadamu duniani.
Tangu kuanza kutolewa kwa tuzo hiyo kuhusu uandishi, waandishi 111 wametuzwa na mwaka huu, mshindi amepata Euro laki Nane.
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2014 atatangazwa leo  Ijumaa jijini Olso nchini Norway.
Patrick Modiano, alizaiwa Julai 30 mwaka 1945 katika mji wa Boulogne-Billancourt. Aliishi katika utoto wake bila kuwa karibu ya mama yake, ambaye alikua mwigizaji, baada ya kuachana na baba yake. Wazazi wa Patrick walikutana mwaka1942 mjini Paris wakati wa uvamizi wa Ujerumani.
Baba yake aliingia kwa siri katika mji wa Paris kwa kuepuka sheria dhidi ya Wayahudi wa utawala wa kiimla. Kifo cha kaka yake Rudy, ambaye alifaraiki mwaka 1957, akiwa na umri wa miaka kumi, ni tukio jingine liliyompa fursa ya kuendelea na kazi ya kuandika vitabu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment