Writen by
sadataley
7:07 PM
-
0
Comments

Ufaransa 2-0 Nigeria
Ufaransa imefuzu kwa mkondo wa
robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuilaza Super Eagles ya Nigeria
mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Brasilia.
Paul Pogba ndiye aliyeifungia Ufaransa bao la
kwanza kunako dakika ya 79 ya mechi hiyo kupitia kichwa baada ya kipa
wa Nigeria Vincent Enyeama kuutema mpira wa kona na kumtnuku Pogba na
fursa ya kuwaweka vijana wa Didier Deschamps mbele.Nigeria itajilaumu yenewe kwa bao hilo kutokana na makosa ya kimsingi ya safu ya ulinzi ambayo haikumakinika katika dakika za mwishomwisho ya mechi hiyo.
Maji yalizidi unga kwa Nigeria ,Dakika chache baadaye Joseph Yobo alipojifunga mwenyewe kufuatia shinikizo la wafaransa Griezmann baada ya Peter Odemwinge kugonga mpira nje na ukawa kona ambayo safu ya ulinzi ilishindwa kuhimili.

Ufaransa sasa itachuana na Ujerumani katika robo fainali ya kombe la dunia
Vile vile kuondolewa kwa mabingwa hao wa Afrika sasa kumeiacha bara zima la Afrika bila ya mwakilishi katika mkondo ujao wa robo fainali baada ya Algeria kufurushwa na Ujerumani katika mechi nyengine 2-1.
Ujerumani ilipata mwaliko huo wa robo fainali baada ya kuibana mwakilishi mwengine wa Afrika Algeria ,mabao 2-1 katika mechi iliyoishia katika mmuda wa ziada .
Mechi hiyo ilikuwa imekamilika suluhu bin suluhu katika muda wa kawaida.
No comments
Post a Comment