Writen by
sadataley
6:54 PM
-
0
Comments

Suarez amuomba msamaha Chiellini kwa mara ya kwanza
Mshambulizi wa Uruguay na
Liverpool ya Uingereza Luiz Suarez sasa amemuomba msamaha mlinzi wa
Italia Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng'ata timu hizo
zilipokuwa zicheza mechi ya mwisho ya makundi huko Brazil.
Suarez aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao
wa Twitter ''baada ya kuketi nyumbani na familia yangu na kutulia
imenijia kuwa tukio la kumng'ata Chellini ni la kusikitisha na kwamba
sitarudia tena .“ninajutia sana tukio hilo na ninamuomba msamaha Chellini .ukweli ni kwamba anauguza jereha la kuumwa baada ya kugongana naye katika mechi hiyo .''
Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.

Suarez amuomba msamaha Chiellini kwa mara ya kwanza
Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia marufuku hiyo.
Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.

Suarez amuomba msamaha Chiellini kwa mara ya kwanza
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.
No comments
Post a Comment