Writen by
sadataley
1:16 PM
-
0
Comments
Waziri Mkuu amesema maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa yameanza lakini kikwazo ni msimamo wa Ukawa katika kupata Katiba Mpya kwa wakati uliopangwa.
Daniel Mjema, Mwananchi
Same. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
amesema Serikali imeshaanza maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mwakani lakini tatizo ni
Katiba Mpya.
Pinda alitoa kauli hiyo jana katika chuo cha ufundi, Kijiji cha Gonja wakati akiweka jiwe la msingi.
“Je, Katiba hiyo Mpya itapita na kama isipopita
je, uchaguzi bado utakuwapo Oktoba au tutausogeza mbele kidogo?” alisema
na kuongeza kuwa changamoto kubwa ni pale Ukawa waliposusa.
“Jitihada zinazoendelea hivi sasa ni kuwataka
warudi kwa sababu mjadala uko bungeni. Pale ambapo itaonekana tuliteleza
tuombane msamaha tusonge mbele”.
“Tubishane lakini tusiwe kikwazo. Kama Ukawa
hawatarudi kimsingi hatuna tatizo kubwa kwa sababu Katiba ya sasa ya
mwaka 1977 itafanyiwa marekebisho madogo ili itumike katika uchaguzi
ujao wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani ili iweze kutuvusha
hapa tulipo,” alisema Pinda bila kutaja aina ya marekebisho
yanayokusudiwa.
Pinda alisema ni vyema ikafahamika kuwa chochote
kile ambacho wajumbe wa Bunge hilo watakubaliana lazima wananchi
watakuwa waamuzi wa mwisho kwa kusema ndiyo au hapana.
No comments
Post a Comment