Writen by
sadataley
2:58 PM
-
0
Comments
Timu ya taifa ya soka ya
Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa na kombe lao la
ushindi walilolinyakua katika mashindano ya kombe la dunia ambyo
yalikamilika juzi nchini Brazil.
Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha wachezaji hao.Sherehe zitafanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambako wachezaji wataonyeshea kombe lao, ambalo walilishinda katika fainali ya mashindano hayo dhidi ya Argentina.
Watu wengi wamenunua jesi zenye nyota nne kuashiria ushindi wa nne wa nchi hiyo katika kombe la dunia.
Mwandishi wa BBC Steve Evans ambaye yuko mjini Berlin anasema kuwa watu nusu milioni wanatarajiwa kukutana na wachezaji hao mjini Berlin.
No comments
Post a Comment