Writen by
sadataley
1:13 PM
-
0
Comments
Zaidi ya wanariadha elfu tatu wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayodumu kwa muda wa majuma matatu yajayo.
Australia ndio nchi ambayo imetuma kikosi kubwa zaidi katika mashindano haya ya mwaka huu.
Takwimu rasmi zinasema kuwa Australia inaakilishwa na zaidi ya wanariadha 400.
Ushindani mkali unatarajiwa katika fani mbali mbali za michezo na macho yote ya dunia itakuwa katika shindano la riadha ambalo litatumiwa na mataifa mengi kuchagua vikosi vyao vitakavyoshiriki katika mashindano ya mabara na hatimaye kombe la dunia.
Mashindano haya yataanza rasmi hiyo kesho huku wanariadha kadhaa wa Afrika Mashariki wakijibwaga ugani kuchuana na wapinzani wao katika raundi ya kwanza ya mashindano ya Judo, Masumbwi na Table tennis.
No comments
Post a Comment