Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 25, 2014

MERIAM IBRAHIM SASA HURU DHIDI YA WATESI, AELEKEA ROMA KUMSABAHI PAPA

Waziri wa mambo ya nje ya Italia, Lapo Pistelli kwenye 'selfie' (picha aliyojipiga) na Meriam, ambapo kwenye mtandao aliandika, 'Mission Accomplished', yaani 'kazi imekamilika.' ©Premier Christian Radio
Hatimaye jasho la haki limepatikana, ambapo Meriam Yahia Ibrahim Ishag, mwanamke aliyepata suluba kutokana na imani yake ameachiwa huru baada ya Vatican kuelezwa kufanya mazungumzo ya chini kwa chini na Sudan na hatimaye kufikia makubaliano.
Meriam amenusuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Italia, Bwana Lapo Pistelli, ambapo hadi kufikia saa kumi alfajiri siku ya Alhamisi, ndege binafsi ilipaa kuelekea Italia, familia ya Meriam ikiwa ndani.
Mara baada ya kufika Roma, Papa Francis ambaye alifurahia uwepo wa watoto wa Meriam na kucheza nao, alimpongeza Meriam kwa kutetea imani na kutotetereka. Kituo cha TV cha Italia kilionyesha ndege iliyombeba ikitua, na kueleza kwamba ataonana na Papa kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea nhini Marekani.
Meriam alihukumiwa kifo baada ya kudaiwa kuikana dini ya Kiislamu na kuwa Mkristo, japo katia maelezo yake ameeleza mara kadhaa kwamba hajawahi kuwa Muislamu, kwani baba yake (ambaye ndiye alikuwa Muislamu) aliitelekeza familia ya kumuachia mama ambaye alikuwa mkristo.
Akiwa kifungoni, Meriama lilazimika kujifungua mtoto wake wa sasa huku akiwa amefungwa kwenye minyororo, jambo ambalo limeelezwa kumsababishia mtoto huyo ulemavu.


Juni 23, Mahakama ya rufaa ilitengua hukumu ya Meriam, na hivyo kumuweka huru, japo maofisa usalama walimkamata upya akiwa uwanja wa ndege kuelekea nchini Marekani, ambapo walieleza kwamba wanakagua hati za kusafiria ambazo zimefojiwa.
Baada ya tukio hilo Meriam aliachiwa na akapata hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani, ambapo ndugu zake walimfungulia kesi upya hadi aliposafiri kwenda 'kumsabahi Papa' kabla ya safari ya Marekani, ambako mume wake ana uraia wa nchi hiyo.
Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment