Writen by
sadataley
1:06 PM
-
0
Comments
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew
amesema kuwa timu yake inapania kuandikisha historia kwa kuwa timu ya
kwanza kutoka bara Uropa kutwaa taji la dunia Kusini mwa Marekani.
Ujerumani itachuana na Argentina katika fainali
ya kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil baadaye Jumapili tarehe 13
Julai katika uwanja wa kihistoria wa Maracana Ulioko mjini Rio de
Jenairo Brazil.Loew anaimani kuwa timu yake itarejesha nyumbani kombe lao la nne la dunia.
“Ninaamini kuwa kikosi hichi kinauwezo wa kuandikisha rekodi ya dunia fauka ya matokeo ya zamani ya timu kutoka barani Uropa''
Hii itakuwa ni mara ya Tatu kwa timu hizo kukutana katika fainali Ujerumani ikishinda mechi moja nayo Argentina ikishinda ile nyengine(1986)
Licha ya hayo ,Loew amemlimbikizia sifa kochokocho kocha mpinzani Alejandro Sabella akisema Argentina ameshinda mechi zao zote licha ya ushindani mkali.
Maonni yake Loew yalitiliwa pondo na kiungo wake wa kati Bastian Schweinsteiger aliyesema kuwa Ujerumani inauwezo wa kuilaza Argentina licha ya wao kuonekana wakakamavu katika safu ya ulinzi.
''Huwezi kuwapuuza washambulizi kama Gonzalo HiguaĆn na Angel Di Maria, ukiwa unadhania Argentina ni Messi umekosea sana''alisema kocha huyo.
No comments
Post a Comment