Writen by
sadataley
6:19 PM
-
0
Comments
Na Elias Msuya, MwananchiDar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeweka bayana mkakati wake mpya wa kushika dola kwa kukita mizizi yake tangu ngazi ya shina hadi ya Taifa.
Mkakati huo, ambao Chadema ilisema unalenga
kukiondoa chama hicho kutoka kwenye uanaharakati na kukifanya kuwa chama
cha dola, umekuja wakati nchi ikijiandaa kwa uchaguzi wa serikali za
mitaa baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa
mwaka ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya
chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema chama hicho tayari kimeunda matawi
196,000 kati ya 250,000 yanayokusudiwa.
“Chadema imeshajiondoa kwenye harakati na kwenda
kuwa chama dola. Tumefanya harakati kwa zaidi ya miaka 20 tukiwa na
lengo la kukipeleka chama kwa wananchi, ili wakielewe na wakiheshimu,
lakini sasa umefika wakati wa kujiandaa kushika dola,” alisema Dk Slaa.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Chadema
ilishika nafasi ya pili kwa kuingiza wabunge wengi huku mgombea wake wa
urais akishika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete, ambaye ushindi wake
ulipungua kutoka zaidi ya asilimia 80 hadi asilimia 61.
Mkakati wa chama
Dk Slaa alisema chama hicho kikuu cha upinzani kwa
sasa kinafanya kazi katika kanda 10, nane zikiwa Bara na mbili Zanzibar
na kanda hizo zimepewa mamlaka hadi ngazi ya chini (msingi).
“Baada ya kuunda kanda hizo 10 kumekuwa na
mafanikio makubwa ambayo ni pamoja na kuunda misingi au mashina. Leo
tuna mabalozi wa nyumba 10 nchi nzima. Mwanachama wetu akipata shida,
hana haja ya kwenda kusuluhishwa na balozi wa CCM,” alisema Dk Slaa na
kuongeza:
“Katika ngazi ya vitongoji tuna matawi au shehia
kule Zanzibar. Lengo letu lilikuwa ni matawi 250,000 hadi sasa tuna
matawi 196,000.”
Dk Slaa alisema kuwa chama hicho kiliahirisha
uchaguzi mkuu mara tatu ili kukijenga kwanza katika ngazi za chini ikiwa
pamoja na kufanya chaguzi katika ngazi hizo.
Akizungumzia uchaguzi wa ngazi ya majimbo, Dk Slaa
alisema ulishaanza tangu Machi 26, mwaka huu na baadhi ya wilaya
zimeshakamilisha.
Aliongeza kuwa baada ya uchaguzi wa majimbo,
utafuata uchaguzi wa wilaya kuanzia Julai 18 hadi 22 utakaofuatiwa na
rufaa kwa wasioridhika na matokeo.
Kwa habari ziaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Chadema-yaibuka-na-mkakati/-/1597296/2385604/-/qt61gdz/-/index.html
Kwa habari ziaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Chadema-yaibuka-na-mkakati/-/1597296/2385604/-/qt61gdz/-/index.html
No comments
Post a Comment