Writen by
sadataley
5:57 PM
-
0
Comments

Mfungaji bao la ushindi la Argentina Di Maria
Argentina ilijikatia tikiti ya robo fainali baada ya ya kusubiri hadi muda wa ziada kuibana Uswisi kwa bao moja kwa nunge.
Timu hizo zilikuwa zimetoka sare tasa katika
dakika 90 za mechi hiyo kabla ya Angel Di Maria kufunga bao la pekee na
la ushindi zikiwa zimesalia dakika mbili za muda huo wa ziada
kukamilika .Bao hilo lilikuwa la 151 katika kipute hichi ikilinganishwa na mabao 145 yaliyofungwa katika kinyang'ari cha miaka minne iliyopita huko Afrika Kusini.
Ijapokuwa nyota wa Barcelona Lionel Messi alikuwa amepigiwa upatu kushamiri katika mechi hii mshambulizi huyo ambaye amefunga bao katika kila mechi alikuwa amekabwa na walinzi wa Uswisi wakiongozwa na Behrami.
Kocha wa Uswisi Ottmar Hitzfeld, alikuwa amepanga kikosi chake kumnyima nafasi yeyote Messi lakini nyota huyo ali geuka na kuwa anagawa mipira alipommegea pasi safi Di Maria .

Mfungaji bao la ushindi la Argentina Di Maria
Granit Xhaka alipoteza nafasi safi ambayo waswisi watajilaumu wenyewe haswa baada ya Josip Drmic kujipata katika hali ya moja kwa moja na kipa wa Argentina Sergio Romero .
juhudi zake hata hivyo ziliambulia mikononi mwa Romero.
Kufuatia ushindi huo Argentina sasa watachuana dhidi ya Ubeljiji katika mechi ya robo fainali ya kombe hilo la dunia jumamosi tarehe 5 Julai .
Ubeliji imejikatia tiketi ya robo fainali hiyo baada ya kuititima Marekani mabao mawili kwa moja katika muda wa ziada wa mechi hiyo ya mwisho ya kundi la 16 bora.
No comments
Post a Comment