Writen by
sadataley
5:01 PM
-
0
Comments

Valencia alioneshwa kadi nyekundu
Ufaransa ilikamilisha mechi za makundi kwa sare tasa dhidi ya Ecuador.
Licha ya sare hiyo Ufaransa ilisalia kileleni
mwa kundi E ikiwa na alama 7 moja zaidi ya Switzerland iliyoisakama Iran
katika mechi ya mwisho.Les Blues walifuzu katika raundi ya 16 bora ambapo sasa watachuana na Nigeria .

Ufaransa itachuana na Nigeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia.
Hadi kufikia hapo Ecuador ilikuwa imepoteza nafasi nyingi tu za wazi Valencia na Cristhian Noboa wakiboronga mbele ya lango.
Ufaransa kwa upande wao pia walinyimwa mabao mengi na kipa machachari wa Ecuador Alexander Dominguez aliyelazimika kufanya kazi ya ziada usiku kucha .

Ufaransa itachuana na Nigeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia.
Ufaransa sasa itakwaruzana na Nigeria waliomaliza mechi yao ya kundi F kwa kushindwa na Argentina kwa mabao 3-2 siku ya Jumatatu tarehe 30 katika Estadio Di Nationale.
Washindi wa kundi hilo Argentina watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Switzerland Jumanne ijayo katika uga wa Arena De Sao Paulo
No comments
Post a Comment