Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, June 29, 2014

SHANGWE ZA GK: KWETU PAZURI YAENDELEA KUWA SEND OFF WAIMBAJI WAKE

Doris akila kiapo cha ndoa katika ofisi ya serikali.
Kwa mara nyingine tena wiki hii katika shangwe za GK tunaye mwimbaji wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda almaarufu kama 'Kwetu Pazuri' aitwaye Doris Kayitesi ambaye wiki hii alikula kiapo cha ndoa kwa upande wa serikalini na mumewe ambaye kwa pamoja wanasubiri ndoa rasmi ya kanisani itakayofanyika hivi karibuni. Mungu amefungua njia kwa waimbaji wa kwaya hiyo ambao wamekuwa wakipata wenzi wao wa maisha, wiki iliyopita ilikuwa Furaha Sandrine ambaye alitolewa mahari pamoja na kuvishwa pete ya uchumba rasmi, wiki hii ni Dorris wengine ni pamoja na kijana Nelson Manzi aliyemtangaza mkewe mtarajiwa hadharani, mwimbaji mwingine anatarajiwa kufunga ndoa na Mtanzania hivi karibuni.
Doris na mumewe mtarajiwa wakionyesha cheti chao baada ya kula kiapo ofisi za serikali.
Wapendanao

Wapendanao ilikuwa ni mapozi ya picha tu.
Doris akiwa na baadhi ya waimbaji wenzake wa Ambassadors.
Inapendeza kuwa pamoja wakati wa raha na shida pia.
Picha hazikutosha kwa furaha ya wana wa Ambassadors.
Matabasamu ya kupendeza, maharusi na waimbaji
Ilikuwa furaha tele. ©Kj Marcello 
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment