Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, January 12, 2014

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yaadhimisha miaka 50 ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar.

Miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar
Miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hii leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka hamsini ya mapinduzi tukufu yaliyomaliza utawala wa Kisultani visiwani humo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ataongoza sherehe hizo ambazo pia zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania bara akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal.
Marais mbali mbali pia wanahudhuria sherehe hizo akiwemo rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais Shein amewataka wananchi kushiriki kikamilifu na kuonesha umoja na mshikamano walionao katika sherehe hizo za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Karume.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment