Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, January 22, 2014

Papa Francis ataka umasikini kutokomezwa

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ametoa wito kwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kimataifa mjini Davos kuhakikisha kuwa mali na utajiri ulio hapa duniani unapaswa kutumiwa kwa njia za kuwanufaisha watu badala ya kuwatawala.
Papa Francis
Papa huyo kutoka Brazil, amekuwa mkosoaji mkubwa wa mfumo wa ubepari ambao unawakandamiza watu walio masikini na amekuwa katika mstari wa mbele kutetea maslahi ya raia wa nchi hiyo ambao wengi wao ni masikini.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba ya papa na Kadinali Peter Turkson, kutoka Ghana, ambaye ni mkuu wa tume ya haki na amani huko Vatican, Papa Francis, amewaomba wafanyabiashara katika mkutano wa kimataifa wa kiuchumi kuusaidia umma, badala ya kuruhusu umaskini usambae duniani.

Kuondoa umasikini duniani

Papa Francis alitoa wito kwa viongozi hao kujitolea zaidi na kufanya mengi zaidi kuliko kuzingatia maslahi ya kawaida na pia kutathmini jinsi ya kuhakikisha kuwa utajiri wa taifa umesambazwa kwa raia wote.
Wakati huo huo amewarai wafanyabiashara kuchukua jukumu hilo huku wakiwa na mtizamo na mwelekeo wa kuimarisha hali ya maisha duniani.
Mapema wiki hii shirika la Oxfam, liliripoti kuwa watu themanini na watano tajiri zaidi duniani, wanamiliki utajiri ambao ni sawa na mali inayomilikiwa na zaidi ya watu bilioni tatu na nusu wengi wao wakijumuisha nusu ya watu walio na mapato ya chini zaidi duniani.
Amesema ukuaji wa usawa ni zaidi ya ukuaji wa kiuchumi licha ya kuwa vyote vinaambatana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment