Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, January 22, 2014

Obama kuzungumzia mwanya unaoongezeka kati ya masikini na matajiri duniani na Papa Francis.

Papa Francis huko Vatican, Jan. 13, 2014.
                                                       Baba Mtakatifu Papa Fracis
Rais Obama.
                                                   Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama atakutana na Papa Francis huko Vatikan wakati wa ziara yake ya wiki moja Ulaya iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa Machi.

White House inasema rais Obama anatarajia kuzungumza na Papa Francis kuhusu mtizamo wao unaolingana katika kupambana na umasikini na tofauti ya kipato inayoendelea kuongezeka.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Machi 27 .Wakati akiwa Roma rais Obama anapanga kukutana na rais wa Italia Giorgio Napolitano  na waziri mkuu Enrico Letta.

Kiongozi huyo wa Marekani ataanza ziara yake ya Ulaya huko The Hague Uholanzi ambako atashiriki katika mkutano wa usalama wa nyuklia ulioandaliwa na serikali ya Uholanzi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment