Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, January 26, 2014

Misri: uchaguzi wa rais utatangulia

Rais wa muda wa Misri, Adly Mansour, amesema uchaguzi wa rais utafanywa kwanza kabla ya uchaguzi wa bunge.
Abdul Fattah al-Sisi
Hayo ni mabadiliko ya utaratibu uliokubaliwa baada ya rais wa Muslim Brotherhood, Mohamed Morsi, kuondolewa madarakani mwaka jana.
Tangazo hilo litazidisha tetesi kwamba mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, atagombea urais.
Jumamosi, maelfu ya watu walikusanyika katika medani ya Tahrir mjini Cairo katika siku ya kuadhimisha miaka mitatu tangu Hosni Mubarak kupinduliwa.
Umati huo ulimtaka Jenerali al-Sisi agombee uongozi.
Wakati huohuo wakuu wamesema watu kama 49 waliuwawa katika sehemu mbali-mbali za nchi, wakati askari wa usalama walipopambana na waandamanaji wanaopinga serikali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment